MITAA YA MPANDA MJINI

Mpanda kama jina ilizaliwa na mto mkubwa ambao hapo zamani uliitwa mto mpanda kwa sasa unapatikana maeneo ya Kigamboni. Mto huo umetupatia leo mji mkubwa sana ambao unazaidi ya wakazi zaidi ya milioni moja ndani ya wilaya tatu wilaya ya mpanda, wilaya ya mlele na wilaya ya tanganyika. zote hizo zikibebwa na mkoa wenye jina la KATAVI. Wilaya ya mpanda ndio makao makuu ya mkoa na ndio mji ambao unaonekan kama kioo cha mkoa kutokana na hatua za kimaendeleo iliyopiga na miradi mikubwa iliomo ndani ya wilaya sambamba za uapatikanaji wa huduma muhimu ndani ya wilaya. Wilaya inamiliki hosipitali ya mkoa, stendi ya mkoa, makoa makuu ya taasisi tofauti tofauti na mashirika makubwa kama shirika la umeme ambalo linahudumia wilaya zote.

Ifuatayo ni mitaa iliomo ndani ya wilaya ya Mpanda mjini

Ukiwa kama mkazi wa mpanda mjini ambaye unaendesha au unategemea kuendesha maisha yako ndani ya mpanda mjini ivi sasa au baadae ni muhimu kufahamu mji wako ili ikusaidie uweze kufahamu sehemu sahihi ambayo utaweza kuishi kulingana na yapatikanayo ndani ya sehemu husika kulingana na upendacho.
1. MAKANYAGIO
Ni moja kati ya mitaa ya kale zaidi kuwepo ndani ya mji wa mpanda. mtaa huu kutokana na ukubwa wake umegawanyika A na B. Mitaa yote miwili hutenganishwa na barabara inayojulikana kama barabara ya pinda inayopita fimbo ya mnyonge mpaka kachoma.
2. MPANDA HOTEL
Mtaa uliokuwa sehemu ya starehe enzi za wakoloni kutokana na uwepo wa hoteli zao na kuupa jina mtaa kama hoteli za mpanda yaani mpanda hoteli, mtaa huu baada ya uhuru na maendeleo ya wilaya ulitengwa kama sehemu ya viwanda. Pamoja na kutengwa kwa matumizi hayo haijazuia muendelezo wa makzi ya watu amabapo bado wananchi wanendelea na ujenzi wa makazi zaidi ya miaka 100 sasa. Pia ndio maa amabo ndani yake una stendi ya treni yaani station.
3. KICHANGANI
Uwingi wa mchanga ndio sababu ya kutokea kw jina la mtaa huo kichangani. Ndio sehemu iliyojulikana wali kama mahali pekee amabapo utapata mchanga wa ujenzi kutokana na uasili wa sehemu hiyo kuwa ni ya kichanga zaidi. Mtaa huu upo pembezoni mwa mji umbali wa 5km kutoka katikati mwa mji.

No comments:

Post a Comment